Kutumia Kivinjari cha Tovuti
Unaweza kuingiza tovuti wakati unapoingiza anwani ya wavuti katika upau wa URL.
Ukiingiza neno la kutafuta, itatafuta maelezo kuhusu neno hilo la kutafuta kutegemea injini ya utafutaji.
  1. Bonyeza kitufe cha MWANZOMWANZO katika kidhibiti cha mbali.
  2. Endesha Kivinjari cha Tovuti programu ya.

Kivinjari cha intanetiKivinjari cha intaneti

  1. Unaweza kuonyesha upya ukurasa wavuti unaotazama.
  2. Unaweza kucharaza anwani ya wavuti ili kuenda kwenye tovuti mahususi au uweke hoja ya kutafuta moja kwa moja.
  3. Unaweza kuona vichupo vilivyo wazi kwa sasa.
  4. Unaweza kuleta karibu au kufifiza wakati wa kuvinjari tovuti.
    Zuia Matangazo : Unaweza kuzuia matangazo ndani ya ukurasa wavuti unaoangalia.
    Hata hivyo, kitufe hiki kinaonyeshwa tu ikiwa kipengele cha Aikoni ya menyuAikoni ya menyu Mipangilio Tumia Zuia Matangazo kimewekwa kuwa Imewashwa.
    Mwonekano wa TV : Gawa skrini ili ionyeshe skrini ya TV. Unaweza kuvinjari kurasa za wavuti unapotazama TV.
    Historia : Unaweza kutazama na kufuta historia ya ziara ya wavuti.
    Ongeza kwenye alamisho : Unaweza kuongeza tovuti unayotazama kwa sasa kwenye Vipendwa vyako.
    Alamisho : Unaweza kutazama na kufuta orodha ya tovuti ulizoongeza kwenye Vipendwa vyako.
    Mipangilio : Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari.
    Mwongozo wa Mtumiaji : Fungua Mwongozo wa Mtumiaji.
    Acha Kutumia Programu : Huzima programu kuacha kufanya kazi chinichini.
  5. Hufunga programu.
  6. Skrini ya kichupo kipya inatoa orodha ya Tovuti Zilizopendekezwa na Tovuti Zilizotembelewa Sana.
    Ikiwa hutaki Tovuti Zilizopendekezwa kuonyeshwa, weka kipengele cha Aikoni ya menyuAikoni ya menyu Mipangilio Onyesha Tovuti Zinazopendekezwa kuwa Imezimwa.
    Tovuti Zilizopendekezwa inaweza kutofautiana na nchi na zinapatikana tu katika nchi fulani.
Programu ya Kivinjari cha Tovuti iliyo kwenye TV yako ni kivinjari cha TV, hivyo huenda kikafanya kazi tofauti na kivinjari cha PC yako.
Tovuti inaweza kufikiwa kupitia programu ya TV ya Kivinjari cha Tovuti, hivyo unapaswa kuwa makini kuhusu ufikiaji wa watoto wa maudhui ya mtandaoni yenye madhara.
Unaweza kufunga programu ya Kivinjari cha Tovuti ili kuzuia ufikiaji wa maudhui ya mtandaoni yenye madhara.
Snidi mipangilio katika MipangilioMipangilio Aikoni ya Mipangilio yoteAikoni ya Mipangilio yote Jumla Mfumo Usalama Makufuli ya Programu.
Ukikumbana na tatizo unapotumia Kivinjari cha Tovuti, rejelea Utatuzi katika Mwongozo wa Mtumiaji.
Kubadilisha Mipangilio ya Kivinjari cha Tovuti
Teua Aikoni ya menyuAikoni ya menyu Mipangilio juu ya programu ya Kivinjari cha Tovuti.
Mwanzo
Unaweza kuchagua ukurasa unaoonekana unapoanzisha programu ya Kivinjari cha Tovuti.
Mitambo ya Kutafuta
Unaweza kuteua mtambo wa utafutaji ili kutafuta wakati wa kuweka nenomsingi katika upau anwani.
Mipangilio ya mtambo wa utafutaji inaweza kubadilishwa bila ilani kulingana na hali za muuzaji.
Onyesha Tovuti Zinazopendekezwa
Unaweza kuweka ikiwa unataka au hutaki kuonyesha orodha ya Tovuti Zilizopendekezwa kwenye skrini ya kichupo kipya.
Onyesha Sehemu ya Anwani Kila Wakati
Inapowekwa kuwa Imewashwa, upau wa anwani na upau wa menyu sehemu ya juu utaonyeshwa kila wakati.
Ripoti ya Otomatiki ya Tatizo la Kivinjari
Wakati imewekwa kuwa Imewashwa, ikiwa kuna hitilafu (haifanyi kazi, hitilafu ya kucheza maudhui, hitilafu ya kupakia ukurasa, kufunga kusiko kwa kawaida, kuchelewa kujibu kutokana na kumbukumbu kidogo, n.k.) hutokea wakati wa kutumia kivinjari, taarifa inayofaa itatumwa kiotomatiki kwa timu ya usanidi wa kivinjari kwenye makao makuu ya LG Electronics (Korea). Taarifa iliyotumwa itatumiwa tu kuboresha utendakazi wa Kivinjari.
Tumia Zuia Matangazo
Wakati imewekwa kuwa Imewashwa, ukibonyeza Aikoni ya menyuAikoni ya menyu juu ya Kivinjari cha Tovuti, kitufe cha kuwasha au kuzima Tumia Zuia Matangazo kitaonekana kwenye skirini. Kuwasha kipengele cha Tumia Zuia Matangazo kunaongeza kasi ya kupakia ukurasa kwa kuzuia matangazo yanayojumuishwa kwenye tovuti.
Kuchuja Tovuti
Unaweza kusajili tovuti ili kuzuia au kuruhusu.
Tovuti Zilizoidhinishwa : Unaweza kusanidi mipangilio ili kufungua kurasa zilizosajiliwa hapo awali peke yake.
Tovuti Ziliozuiwa : Unaweza kusanidi mipangilio kuzuia tovuti mahususi.
Ili kutumia utendaji wa Kuchuja Tovuti unapaswa kuingiza nywila la televisheni.
Kizuiaji cha Ibukizi
Inazuia ibukizi zinazoonyeshwa kiotomatiki na kurasa wavuti.
Kuvinjari kwa Faragha
Ikiwa imewekwa kuwa Imewashwa, haitaacha historia ya ziara za tovuti.
Usifuatilie
Unaweza kuomba tovuti kutoacha historia ya ziara yako. Shughuli inaweza kutofautiana kutegemea na sera ya tovuti.
Utiririshaji wa Kubadilika kwa kutumia JavaScript
Teknolojia ya kutiririsha midia kwa kutumia JavaScript hukuruhusu kutazama video kwa ubora ulioimarishwa.
Hali hii ikiwekwa kuwa Imezimwa, ubora wa kucheza video za Kivinjari cha Tovuti utakuwa 720p tu.
Mipangilio ya Vidakuzi
Inawezesha tovuti kuhifadhi na kutumia data ya vidakuzi.
Futa Data ya Kuvinjari
Futa Vidakuzi : Hufuta data ya vidakuzi. Inapofutwa, unaondolewa kwenye tovuti nyingi.
Futa Data Yote ya Kuvinjari : Hufuta historia yote ya kuvinjari, ikiwemo vidakuzi.