Kuunganisha kwenye Mtandao
Ukisanidi mipangilio ya mtandao, unaweza kutumia huduma mbalimbali kama vile maudhui ya mtandaoni na programu.
Kuweka Mtandao wa Waya
-
Unganisha tundu la LAN la televisheni na kielekezi kwa kutumia kebo.
Kielekezi kinapaswa kuunganishwa kwenye Intaneti kabla.Unapounganisha televisheni kwa mtandao ukitumia kebo ya LAN, televisheni huunganishwa kiotomatiki kwenye mtandao ikiwa kielekezi kinatumia DHCP. -
Bonyeza kitufe cha
katika kidhibiti cha mbali.
-
Chagua
Jumla Mtandao Muunganisho Ulio na Waya (Ethaneti).
Ili kuona maelezo, bofya Mipangilio Mtandao Muunganisho Ulio na Waya (Ethaneti) katika Mwongozo wa Mtumiaji.
Ikiwa mtandao haujaunganishwa kiotomatiki
Kuweka Mtandao Pasiwaya
- Washa kielekezi kilichounganishwa kwenye Intaneti.
-
Bonyeza kitufe cha
katika kidhibiti cha mbali.
-
Chagua
Jumla Mtandao Muunganisho wa Wi-Fi.
- Utafutaji wa mtandao utakapokamilika, orodha ya mitandao inayopatikana kwa ajili ya muunganisho itaonyeshwa.
-
Chagua mtandao wa kuunganisha.
Kama Kielekezi chako cha LAN cha pasi waya kimelindwa kwa nywila, ingiza nywila lililosanidiwa kwa kielekezi.
Ili kuona maelezo, bofya Mipangilio Mtandao Muunganisho wa Wi-Fi katika Mwongozo wa Mtumiaji.
Onyo Kuhusu Mipangilio ya Mtandao
Tumia kebo ya kawaida ya LAN (unganisha kwa Cat7 au aina ya juu ukitumia kiunganishi cha RJ45, lango la 10 Base-T, au 100 Base TX LAN).
Kuweka upya kisambaza data kunawza kusababisha matatizo ya muunganisho wa mtandao.
Katika hali hii, kisambaza data kitatumika kawaida ukikizima na kutenganisha TV na kisha kuunganisha tena na kukiwasha.
Mtengenezaji hawajibikii muunganisho wa mtandao au hitilafu wa kutotumika kutokana na matatizo kama vile hitilafu ya kifaa au laini zilizotenganishwa.
Huenda muunganisho kwenye mtandao usifanye kazi vizuri kutokana na mipangilio ya mtandao au mtoa huduma za Intaneti.
Huduma ya DSL lazima itumie modemu ya DSL na huduma za kebo lazima zitumie modemu ya kebo. Kwa kuwa ni miunganisho michache tu ya mtandao ambayo huenda inapatikana, huenda mipangilio ya mtandao wa televisheni usitumike kutegemea mkataba uliopo na mtoa huduma za Intaneti. (Kama mkataba haukubalii zaidi ya kifaa kimoja kwa kila laini, ni kompyuta iliyounganishwa tayari ambayo inaweza kutumiwa.)
Mtandao usiotumia nyaya unaweza kutatizwa na vifaa vingine ambavyo hutumia masafa ya 2.4 GHz (simu ya mkononi, kifaa cha Bluetooth, au jiko la maikrowevu). Ingawa matatizo yanaweza kutokea unapotumia masafa ya 5 GHz, litakuwa jambo la nadra sana.
Mazingira ya vifaa vya pasi waya yanaweza kufanya huduma ya mtandao usiotumia nyaya kufanya kazi polepole.
Kutumia vifaa mbalimbali vya pasiwaya kwa wakati mmoja kunaweza kupunguza kasi ya mtandao wako.
Kifaa cha kufikia mtandao sharti kiwe na uwezo wa kutumia miunganisho wa pasi waya na kipengee cha kuunganisha bila nyaya sharti kiwezeshwe kwenye kifaa ili kuwa na muunganisho wa AP (kituo cha kufikia). Wasiliana na mtoa huduma kwa upatikanaji wa miunganisho isiyotumia nyaya katika kituo cha ufikiaji.
Angalia SSID na mipangilio ya usalama ya AP. Rejelea hati zinazofaa kwa SSID na mipangilio ya usalama wa AP.
Ikiwa mtandao umebadilika kwa kusogeza TV au kubadilisha ruta, lazima uweke mtandao wa pasiwaya tena.
Miunganisho ya mtandao pasiwaya iliyopo haitahifadhiwa.
Mipangilio isiyo sahihi ya vifaa vya mtandao (kishiriki laini kinachotumia nyaya/pasi waya, habu) inaweza kufanya televisheni kufanya kazi polepole au isifanye kazi vizuri. Sakinisha vifaa kwa njia nzuri kulingana na mwongozo unaofaa na mtandao.
Njia ya muunganisho inaweza kutofautiana kutegemea mtengenezaji wa AP.
Ili kutatua tatizo linalihusiana na utendaji huu, rejelea sehemu ya Utatuzi ya Mwongozo wa Mtumiaji.