Kutazama Skrini ya Vifaa Mahiri kwenye TV
- Wezesha hali ya Screen Share kwenye kifaa mahiri.
- Televisheni yako itaonyeshwa kwenye orodha ya vifaa vinavyopatikana.
- Chagua runinga yako kisha uombe muunganisho.
- Chagua Kubali katika kidirisha cha idhini kitakachotokea.
- Baada ya muunganisho kupatikana, televisheni itaonyesha skrini ya kifaa kilichounganishwa.
Unapounganisha Screen Share kwa mara ya kwanza, ibukizi itaonekana ambayo inakuruhusu kuteua Kubali, Kataa au Zuia.
- Kubali : Unaweza kuunganisha kifaa. Hakuna ibukizi ya muunganisho itakayoonekana kwa mara ya pili.
- Kataa : Usiunganishe kifaa. Ukijaribu kuunganisha tena, ibukizi itaonekana.
-
Zuia
:
Usiunganishe kifaa.
Hata ikiwa unajaribu kuunganisha tena, ibukizi haitaonekana na muunganisho hautafanya kazi.
Ili kuzima Zuia, nenda kwenye
Jumla Vifaa Vifaa vya Nje na uteue Futa Historia ya Muunganisho.
Kwa muunganisho wa kutegemewa, kila mara, hakikisha kifaa kilichounganishwa kwenye televisheni yako kimesasishwa hadi toleo la hivi karibuni la OS.
Kutegemea muundo au mtengenezaji wa kifaa mahiri, huenda kipengele cha Screen Share kisitumike.
Unganisha kifaa na kielekezi cha 5 GHz kwa sababu utendaji unaweza kuathiriwa na mazingira kilipo kifaa chako kisichotumia nyaya.
Kiwango cha kutumika kinaweza kutofautiana kutegemea mazingira ya mtumiaji.
Hutofautiana miongoni mwa vifaa. Unapojaribu kuunganisha kwenye kifaa, rejelea mwongozo wa matumizi kwa maelezo zaidi.
Muunganisho ukikosekana mara kwa mara, zima televisheni na kifaa unachojaribu kuunganisha. Kisha ziwashe na ujaribu tena.