Tazama maudhui yaliyohifadhiwa katika PC yako kwenye TV
Unaweza kufurahia video/muziki/picha zilizohifadhiwa kwenye PC yako kwenye TV wakati vifaa hivi vinaunganishwa kwenye mtandao sawa.
Vinjari maudhui kwenye PC yako ili kutazama kwenye TV (Windows 10)
- Unganisha TV na kompyuta yako kwenye mtandao mmoja.
- Bofya kulia kwa faili unayotaka kucheza na uteue “Tuma kwenye Kifaa”.
- Teua jina la TV unayotaka kutazama kutoka kwenye orodha inayoonyeshwa na kucheza kutaanza kwenye TV hiyo.
Hata pale mbapo televisheni au vifaa vingi vimeunganishwa, faili iliyochaguliwa itachezwa kupitia kifaa kimoja tu. Kiwango cha urudiaji video kinaweza kutofautiana kutegemea muunganisho wa mtandao.
Ili kucheza kwenye mifumo mingine ya uendeshaji au vifaa, rejelea mwongozo wa mfumo wa uendeshaji/kifaa.
Vinjari na utazame maudhui yaliyohifadhiwa kwenye PC kwa kutumia TV (Windows 10)
- Unganisha TV na kompyuta yako kwenye mtandao mmoja.
- Fungua menyu ya “Anza” kwenye skrini ya PC yako, tafuta “machaguo ya kutiririsha maudhui” kisha uteue matokeo yanayoonekana.
- Teua kitufe cha “Washa utiririshaji maudhui” katika dirisha linalofunguka.
- Ruhusu “machaguo ya kutiririsha maudhui”.
- Teua “Sawa” ili kuhifadhi mipangilio.
- Teua PC iliyounganishwa katika programu ya Dashibodi ya Nyumbani kwenye TV kisha uteue na ucheze faili unayotaka.
Ili kucheza kwenye mifumo mingine ya uendeshaji au vifaa, rejelea mwongozo wa mfumo wa uendeshaji/kifaa.
Maswala ambayo yanahitaji kuzingatiwa kwa makini wakati wa Kushiriki Maudhui
Angalia mipangilio yako ya mtandao kama chaguo la Kushiriki Maudhui halifanyi kazi vizuri.
Huenda isifanye kazi vizuri katika mtandao wa pasi waya. Inapendekezwa kwamba uunganishe na mtandao unaotumia nyaya.
Huenda isifanye kazi vizuri kutegemea mazingira ya mtandao.
Kama televisheni kadhaa zimeunganishwa kwenye kifaa kimoja, huenda maudhui yasichezwe vizuri kutegemea utendaji wa seva.
Ili kutazama video ya 1080p kupitia kipengele cha kushiriki maudhui, kisambaza data kinachotumia masafa ya 5 GHz kinahitajika.
Ukitumia kisambaza data kilichopo cha 2.4 GHz, video inaweza kucheza polepole au kutocheza vizuri.
Huenda utendaji wa Kushiriki Maudhui hautumiki kwa kielekezi kisichotumia maonyesho mengi. Kwa maelezo zaidi, rejelea mwongozo wa mtumiaji ulikuja na kielekezi au uwasiliane na mtengenezaji kielekezi.
Manukuu yanatumika tu katika baadhi ya vifaa vilivyounganishwa.
Ikiwa umeongeza faili ya manukuu baadaye, lemaza folda inayoshirikiwa kwenye PC na kisha uiwezeshe tena.
Faili za DRM zilizo katika kifaa kilichounganishwa hazitacheza.
Hata kwa umbizo la faili linalotumika kwenye televisheni, umbizo la faili lialotumika linaweza kutofautiana kutegemea mazingira ya kifaa kilichounganishwa.
Kuna kabrasha au faili nyingi sana katika kabrasha, huenda isifanye kazi vizuri.
Maelezo yaliyo kwenye faili iliyoletwa kutoka kwenye kifaa kilichounganishwa huenda yasionyeshwe kwa njia sahihi.
Kutegemea usimbaji, huenda baadhi ya mipasho isicheze katika modi ya Kushiriki Mudhui.