Sasisho la Programu
MipangilioMipangilio Aikoni ya Mipangilio yoteAikoni ya Mipangilio yote Usaidizi Sasisho la Programu
Hutumia sasisho la programu kuangalia na kupata matoleo y hivi karibuni.
Sasisho Otomatiki
Inapowekwa kuwa Imewashwa, masasisho yanafanywa kiotomatiki bila utaratibu tofauti wa thibitisho isipokuwa kwa baadhi ya masasisho muhimu.
Angalia Masasisho
Wakati wa,kuangalia toleo la hivi karibuni la sasisho, unaweza kusasisha tu wakati faili ya sasisho la hivi karibuni inapatikana. Televisheni huangalia kiotomatiki toleo la programu zako lakini ikibidi, unaweza kujiangalilia mwenyewe.
Vipengee vya kusanidiwa hutofautiana kutegemea modeli.
Toleo la hivi karibuni linaweza kupatikana kupitia ishara za matangazo ya kidijitali au kupitia miunganisho ya Intaneti.
Kubadilisha kituo wakati unapopakua programu kupitia ishara ya utangazaji wa kidijitali hutatiza mchakato wa kupakua. Kurejea kwenye kituo ca awali huruhusu upakuaji kuendelea.
Kama programu haijasasishwa, baadhi ya utendaji huenda usifanye kazi vyema.
Katika baadhi ya nchi, Sasisho Otomatiki haionyeshwi ikiwa hujaunganisha kwenye Intaneti.