Kuchagua Hali ya Picha
MipangilioMipangilio Aikoni ya Mipangilio yoteAikoni ya Mipangilio yote Picha Teua Modi
Chagua hali ya picha inayofaa zaidi mazingira unapotazamia, mapendeleo yako au aina ya video.
Teua hali ya picha. Kwa kurekebisha na kuweka kila kipengee kwa kina zaidi kulingana na hali, video yako inaboreshwa zaidi kwa sifa zake.
Vipengee vya kusanidiwa hutofautiana kutegemea modeli.
Unapotumia mawimbi ya kawaida
Dhahiri
Huboresha picha kwa kuongeza utofautishaji, ung’aavu na umadhubuti.
Kawaida
Huonyesha picha zikiwa na viwango vya kawaida vya utofautishaji, ung’aavu na umadhubuti.
Eco / APS
Kipengele cha Kikokoa Umeme hubadilisha mipangilio ya runinga ili kupunguza matumizi ya umeme.
Vipengee vya kusanidiwa hutofautiana kutegemea modeli.
Sinema
Skrini imeboreshwa ili kufaa utazamaji wa filamu.
Spoti / Soka / Cricket
Skrini imeboreshwa ili kufaa utazamaji wa michezo. Huboresha umadhubuti wa picha zinazossogea kw akasi kama vile kupiga au kurusha mpira.
Jina la mchezo linaweza kuwa tofauti kutegemea nchi.
Kiboreshaji Michezo
Skrini imeboreshwa ili kufaa uchezaji wa michezo ya video.
Unapotumia mawimbi ya HDR/Dolby Vision
Dhahiri
Huboresha picha kwa kuongeza utofautishaji, ung’aavu na umadhubuti.
Kawaida
Katika mazingira ya kawaida ya kutazama, itafungua skrini inayoweza kuonyesha ubora na ung’aavu wa HDR.
Sinema
Skrini imeboreshwa ili kutumia mawimbi ya video ya HDR.
Kiboreshaji Michezo
Skrini imeboreshwa ili kufaa uchezaji wa michezo ya video.
Video ya ubora wa HDR/Dolby Vision ikiwekwa katika runinga ambazo haziwezi kutumia teknolojia ya HDR/Dolby Vision, mitindo ya picha ya kawaida hutumiwa.
Hali za picha zinaweza kuwa tofauti kutegemea mawimbi ya maudhui.
Wakati unapotazama maudhui ya mtandaoni, Hali ya Picha inaweza kubadilishwa ili kulingana na maudhui yanayoonyeshwa.
Mabadiliko ya Teua Modi yanaweza kubadilisha mipangilio ya Kuhifadhi Nishati na yanaweza kuathiri matumizi ya nishati. Unaweza kubadilisha mipangilio katika Jumla Kuhifadhi Nishati.