Kurekebisha Ung`aavu wa Picha
Picha
Mipangilio ya Kiwango cha Juu
Ung’aavu
Unaweza kurekebisha ung’aavu wa skrini nzima.
- Ung`aavu wa Kidirisha
-
Hudhibiti kiasi cha ung’aavu wa skrini na kurekebisha mwanga wa skrini. Kadri inayokaribia 100 ndivyo inavyong’aaa zaidi.
Punguza Ung`aavu wa Kidirisha ili upunguze matumizi ya umeme.Kutegemea Kuhifadhi Nishati (Oto/Kiwango cha juu), huenda hutaweza kubadilisha Ung`aavu wa Kidirisha.
Katika hali hii, nenda kwenye
Jumla Kuhifadhi Nishati Hatua ya Kuokoa Nishati kisha uweke Imezimwa au Kiwango cha chini.
Kutegemea na modeli ya TV yako, huenda isiwe na mipangilio ya Ung`aavu wa Kidirisha. - Ung`aavu wa Pikseli ya OLED
-
Hurekebisha ung’aavu wa skrini kwa kubadilisha ung’aavu katika paneli ya OLED.
Kutegemea Kuhifadhi Nishati (Oto/Kiwango cha juu), huenda hutaweza kubadilisha Ung`aavu wa Pikseli ya OLED.
Katika hali hii, nenda kwenye
Jumla OLED Care Huduma Binafsi ya Kifaa Kuhifadhi Nishati Hatua ya Kuokoa Nishati kisha uweke Imezimwa au Kiwango cha chini.
Kutegemea na modeli ya TV yako, huenda isiwe na mipangilio ya Ung`aavu wa Pikseli ya OLED. - Rekebisha Ulinganuzi
- Hurekebisha utofautishaji wa rangi katika sehemu zenye ung’aavu na zenye giza kwenye picha. Ikiwa karibu na 100, utofautishaji huwa wa juu zaidi.
- Kiwango cha Weusi
- Hurekebisha ung`aavu wa sehemu zenye giza za skrini. Kadri inavyokaribia 100, ndivyo skrini inavyokuwa nyepesi.
- Ulinganuzi wenye Nguvu Kiotomatiki
- Husahihisha tofauti iliyopo kati ya sehemu zenye mwangaza na zisizo na mwanga kwenye skrini ili kuboresha taswira kulingana na ung’aavu wa picha.
- Gama(Rekebisha Ung`aavu)
-
Hurekebisha ung’aavu wa katikati katika picha.
BT.1886 huonyesha daraja katika ITU-R BT.1886, ambacho ni kiwango cha kimataifa.
- Masafa ya Video
-
Hurekebisha giza la skrini ili kuonyesha weusi bora.
Teua Masafa ya Video ili kulinganisha masafa ya rangi ya kifaa cha ingizo la ndani.
Kipengele hiki kinaweza kutumiwa unapotazama maudhui kupitia ingizo la nje.
Chaguo zilizopo zinaweza kuwa tofauti kutegemea chanzo cha mawimbi au hali ya picha iliyochaguliwa.
Vipengee vya kusanidiwa hutofautiana kutegemea modeli.