Kuweka Mtandao wa Waya
MipangilioMipangilio Aikoni ya Mipangilio yoteAikoni ya Mipangilio yote Jumla Mtandao Muunganisho Ulio na Waya (Ethaneti)
Ikiwa kisambaza data kilichounganishwa kwenye mtandano kinatumia kipengele cha DHCP, kuunganisha TV na kisambaza data kwa waya kutaunganisha kwenye mtandao kiotomatiki. Ikiwa haitumii usanidi wa kiotomatiki, unaweza kuteua Hariri ili kusanidi muunganisho wako wa mtandao kiotomatiki.
Kuweka Mtandao Pasiwaya
MipangilioMipangilio Aikoni ya Mipangilio yoteAikoni ya Mipangilio yote Jumla Mtandao Muunganisho wa Wi-Fi
Kama umeiweka TV yako iweze kutumia mtandao pasiwaya, unaweza kutafuta na kuunganisha kwenye mitandao ya Intaneti inayopatikana. Teua kisambaza data pasiwaya ili uunganishe.
Kwa mipangilio ya kina zaidi, teua Mipangilio Mengine ya Mtandao.
Ongeza mtandao fiche pasiwaya
Unaweza kuongeza mtandao pasiwaya kwa kuweka jina la mtandao moja kwa moja.
Unganisha kupitia WPS PBC
Ikiwa kisambaza data pasiwaya unachotaka kuunganisha kwacho kina kipengele cha Wi-Fi Protected Setup-Push Button Configuration (WPS-PBC), unaweza kuunganisha kwa urahisi kwenye kisambaza data pasiwaya kwa kubonyeza kitufe cha WPS-PBC kwenye kisambaza data. Bonyeza kitufe cha kisambaza data cha WPS-PBC kisha ubonyeze kitef cha TV cha [Unganisha].
Unganisha kupitia WPS PIN
Hii ni mbinu ya kuunganisha kwenye eneo la ufikiaji ukitumia Wi-Fi Protected Setup-Personal Identification Number (WPS-PIN). Teua eneo la ufikiaji (AP) ambalo ungependa kuunganisha. Weka PIN inayoonyeshwa kwenye kifaa cha Wi-Fi cha eneo la ufikiaji.
Mipangilio ya kiwango cha juu ya Wi-Fi
Pindi tu unapounganisha kwenye mtandao pasiwaya unaweza kutazama taarifa ya muunganisho kama vile taarifa ya kina ya anwani ya IP. Mbali na hayo, unaweza kubadilisha anwani ya IP na anwani ya seva ya DNS unayotaka kuunganisha kwayo kwa kubonyeza kitufe cha Hariri.
Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuunganisha kwenye mtandao, tazama Kuanza Kutumia webOS TV Kuunganisha kwenye Mtandao katika Mwongozo wa Mtumiaji.