Kutumia Utendaji wa TV kupitia kipengele cha Kutamka
Unaweza kufikia vipengele vya utendaji vya TV kwa urahisi na hara kupitia kipengele cha utambuzi wa usemi.
  1. Bonyeza na ushikilie kitufe cha MaikrofoniMaikrofoni kwenye kidhibiti mbali utamke utendaji unaotaka kuanzisha au neno muhimu unalotaka kutumia kwa utafutaji wako.
  2. Ukiachilia kitufe cha MaikrofoniMaikrofoni baada ya kuingiza usemi wako, utendaji unaolingana utaanzishwa.

Utambuzi wa sautiUtambuzi wa sauti

Huenda baadhi ya modeli zisitumike.
Lugha ya Menyu (Menu Language) lazima iwekwe kuwa lugha rasmi ya nchi katika Eneo ili kuona matokeo sahihi ya utafutaji. Ikiwa Lugha ya Menyu (Menu Language) haijawekwa kuwa lugha rasmi, huenda vipengele vingine vikawa na kikomo.
Unaweza kubadilisha lugha katika MipangilioMipangilio Aikoni ya Mipangilio yoteAikoni ya Mipangilio yote Jumla Mfumo Lugha (Language) Lugha ya Menyu (Menu Language).
Lugha zinazopatikana kwa vipengele vya utambuzi wa sauti zinaweza kubadilishwa kulingana na Sera ya Uendeshaji Huduma.
Maelezo ya huduma yanaweza kutofautiana kulingana na modeli.
Tafadhali fahamu kwamba huduma zinazowezesha amri za matamshi, utambuaji wa sauti na vipengele vingine mahiri zinaweza kubadilishwa, kuondolewa au kusitishwa, bila ilani, na mtengenezaji au watoa huduma wake wengine.
Unaweza kubadilisha mipangilio inayohusiana na sauti au kuona vipengele vilivyopo ili kutumika pamoja na sauti katika MipangilioMipangilio Aikoni ya Mipangilio yoteAikoni ya Mipangilio yote Jumla Huduma ya AI Mipangilio ya Utambuzi wa Sauti/Usaidizi wa Utambuzi wa Sauti.
Tahadhali za Utambuzi wa Sauti
Utambuzi wa sauti huhitaji Magic Remote, ambayo huenda hatumiki katika baadhi ya modeli.
Ili kutumia vipengee vyote vya kutambua matamshi, unahitajika kuweka idhaa, eneo lako n.k. La sivyo, huwezi kutumia baadhi ya vipengele.
Lazima uwe na mtandao ili utumie kipengele cha utambuzi wa matamshi.
Kama una muunganisho wa mtandao, unahitajika kukubaliana na sheria na masharti ili kutumia huduma ya kutambua sauti.
Ili kudhibiti king`amuzi kilichounganishwa kwenye TV kwa kipengele cha kutambua sauti, nenda kwenye MipangilioMipangilio Aikoni ya Mipangilio yoteAikoni ya Mipangilio yote Jumla Vifaa Vifaa vya Nje Mipangilio ya Udhibiti Jumla ili uweke Universal Control.
Inapendekezwa kuelekeza Magic Remote upande wa king’amuzi baada ya ingizo la sauti.
Kiwango cha utambuzi wa sauti kinaweza kutofautiana kutegemea sifa za mtumiaji (ukubwa wa sauti, matamshi, lafudhi na kasi ya kuzungumza) na mazingira (kelele na ukubwa wa sauti ya TV).
Ili kutambua sauti yako kwa njia sahihi, lazima utamke maneno taratibu na kwa njia sahihi ukitumia ukubwa wa sauti unaofaa kwa umbali wa sentimita 10 hivi (Inchi 4) kutoka kwa maikrofoni ya Magic Remote.
Kama sauti yako haitatambuliwa vyema, huduma ya utambuzi wa sauti inaweza kufanya kazi kwa njia tofauti na jinsi ulivyonuia.