Kutumia puku cha USB Kinachotumia Nyaya/Isiyotumia Nyaya
Unganisha puku chako kwenye shimo la USB. Tumia puku kuashiria skrini ya televisheni na uchague menyu unayoitaka.
Kitufe cha upande wa kulia na vitufe maalum vilivyo kwenye puku havifanyi kazi.
Unapotumia kipanya cha USB pasiwaya, muunganisho unaweza kupotea au kupungua, kutegemea na umbali baina ya TV na kipanya na mazingira pasiwaya.
Kutumia Kibodi ya USB Inayotumia Nyaya/Isiyotumia Nyaya
Unganisha kibodi yako kwenye shimo la USB. Unaweza kuingiza maandishi kwa kutumia kifaa cha kibodi kilichounganishwa.
Haiwezekani kuingiza maandishi katika baadhi ya skrini.
Inapendekezwa kwamba utumie bidhaa ambazo zimefanyiwa majaribio na kuonekana kwamba zinaingiliana na TV.
Logitech K360, Logitech K400, Logitech K750
Unaweza kubadilisha lugha kwa kubonyeza kibonye cha kubadilisha lugha au kibonye cha Alt kilicho kulia. Pia unaweza kubadilisha kwa kubonyeza kibonye cha Ctrl na kibonye cha nafasi wakati mmoja.
Unapotumia kibodi ya USB pasiwaya, muunganisho unaweza kupotea au kupungua, kutegemea na umbali baina ya TV na kibodi na mazingira pasiwaya.
Ili kuingiza maandishi katika sehemu ya kuweka maandishi, tumia kibodi ya kwenye-skrini au kibodi ya USB.
Kutumia padi ya michezo
Unganisha padi yako ya michezo katika shimo la USB lililo katika televisheni yako ikiwa mchezo unahitaji padi ya michezo.
Inapendekezwa kwamba utumie bidhaa ambazo zimefanyiwa majaribio na kuonekana kwamba zinaingiliana na TV.
Sony DualShock 4, Sony DualShock 3, Kidhibti cha Microsoft Xbox 360, Kidhibti cha NVIDIA SHIELD, Logitech F310, Logitech F710
Kuunganisha Vifaa vya Ingizo la Bluetooth
Unaweza kuunganisha na kutumia vifaa kama vile kibodi, kipanya au padi ya michezo yenye Bluetooth na TV yako.
Ili kuona maelezo, bofya Mipangilio Vifaa Vifaa vya Nje Unganisha Kidhibiti cha Bluetooth katika Mwongozo wa Mtumiaji.