Kutumia Sauti kuwa Matini
Unaweza kuandika matini katika sehemu za matini kwa kutumia kipengele cha kutambua sauti.
Chagua kitufe cha MaikrofoniMaikrofoni kwenye skrini ya kibodi ili ubadilishe uanze kutumia hali ya kuingiza usemi.
Huenda baadhi ya modeli zisitumike.
  1. Sogeza kiashiria cha Magic Remote katika kisanduku cha kuweka maandishi ili ufungue kibodi pepe.

    Fungua kibodi pepeFungua kibodi pepe

  2. Bofya kitufe cha MaikrofoniMaikrofoni kwenye kibodi pepe.
  3. Baada ya kidirisha cha kutambua sauti kufunguka inavyoonyeshwa hapa chini, zungumza polepole na kwa utaratibu kwenye maikrofoni ya kidhibiti cha mbali.

    Onyesho la Maelezo ya Sauti kuwa MatinisOnyesho la Maelezo ya Sauti kuwa Matinis

    Zungumza na Magic RemoteZungumza na Magic Remote

  4. Ikiwa kuna maneno yanayofanana na uliyotamka kwa sauti, huenda uone orodha ya matokeo kadhaa kama ilivyoonyeshwa hapana chini. Usipopata matokeo unayotaka, bonyeza JARIBU UPYA ujaribu tena. Chagua matokeo na yataonyeshwa kwenye kisanduku cha matini.

    Orodha ya Matokeo ya Sauti kuwa MatiniOrodha ya Matokeo ya Sauti kuwa Matini

Tahadhari unapotumia Sauti kuwa Matini
Angalia muunganisho wa mtandao kabla ya kutumia Sauti kuwa Matini.
Unaweza kubadilisha lugha katika MipangilioMipangilio Aikoni ya Mipangilio yoteAikoni ya Mipangilio yote Jumla Mfumo Lugha (Language) Lugha ya Menyu (Menu Language). Ili kubadilisha kwa muda mfupi hadi lugha nyingine ya utambuzi wa sauti, bonyeza kitufe cha NyekunduNyekundu kilicho katika dirisha la kuonyesha utambuzi wa sauti.
Unaweza kutumia utendaji huu tu baada ya kukubaliana na sheria za Utambuzi wa Sauti.
Gharama ya Sauti kuwa Matini inaweza kutofautiana kutegemea sifa za mtumiaji (sauti, matamshi, kiimbo,na kasi ya kusema) na mazingira (kelele na ukubwa wa sauti ya televisheni).
Ili kuboresha usahihi wa Sauti kuwa Matini, lazima uzungumze kwa uwazi na kwa sauti ukiwa takribani centimita 10 (inchi 4) kutoka kwenya maikrofoni ya Magic Remote.
Huduma ya utambuzi wa sauti haipatikani katika sehemu yoyote inayohitaji uingize nywila na upau wa kuweka anwani ya Kivinjari cha Tovuti yako (haijumuishi utafutaji wa kawaida).