Inasakinisha programu
Unaweza kusakinisha programu katika kategoria mbalimbali kama vile michezo, elimu na habari na kuzitumia kwenye TV yako kwa urahisi.
  1. Bonyeza kitufe cha MWANZOMWANZO katika kidhibiti cha mbali.
  2. Inaanzisha Apps.
  3. Teua kategoria au bonyeza kitufe cha TafutaTafuta ili utafute programu.
  4. Teua programu ili usakinishe.
  5. Soma maelezo kuhusu programu kisha ubonyeze Sakinisha.
  6. Ikimaliza kusakinisha, unaweza kutumia programu mara moja.

AppsApps

  1. Utafutaji wa maudhui.
    Ili kuona maelezo, bofya Programu na Maudhui Utafutaji wa Maudhui katika Mwongozo wa Mtumiaji.
  2. Unaweza kuingia kwenye akaunti yako ya LG.
  3. Unaweza kudhibiti programu, kama vile kusasisha au kufuta programu zilizosakinishwa.
  4. Hufunga programu.
    Ili kuzima programu kuacha kufanya kazi chinichini, bonyeza kitufe cha Vitendo ZaidiVitendo Zaidi kwenye kidhibiti mbali na uteue Acha Kutumia Programu.
Ili kusakinisha programu, lazima uwe umeingia.
Kategoria zilizopo zinaweza kutofautiana kutegemea nchi na hali ya huduma.
Kama hifadhi katika televisheni yako haitoshi, unaweza kusakinisha programu kwa kuiunganisha na kifaa cha hifadhi ya nje.
Baadhi ya vifaa vya hifadhi vya USB huenda havitumiki au huenda havifanyi kazi vizuri.
Hifadhi ya USB iliyo na programu kutoka TV zingine huenda isitumike.
Kuwa mwangalifu wakati ukurasa unapotumiwa na watoto. Watoto waanaweza kufikia maudhui yasiyofaa mtandaoni kupitia bidhaa hii. Unaweza kuzuia maudhui ya mtandaoni yasiyofaa kwa kudhibiti ufikiaji kwenye baadahi ya programu.
Snidi mipangilio katika MipangilioMipangilio Aikoni ya Mipangilio yoteAikoni ya Mipangilio yote Jumla Mfumo Usalama Makufuli ya Programu.